Spread the love

Suala zima la kutafuta tenda katika kampuni husika linamhusisha kila mmoja kwani upatikanaji wa tenda hizo ndo huakikisha kwamba kampuni inaingiza kipato cha ktosha na kuendelea. Kwa mantiki hiyo kila kampuni inakuwa na taratibu zake nyingi nyingi ili kuhakikisha kwamba mwisho wa siku inajipatia tenda za kutosha. Lakini kati kati ya harakati hizi wazabuni au watafuta tenda wanakutana na changamoto nyingi sana ambazo kwa namna moja au nyingine zinawakwamisha katika kutimiza majukumu yao, na moja ya changamoto hizo ikiwa kama ifuatavyo;

Kukosa ushirikiano kutoka katika ofisi za watangaza tenda wakati wa ukusanyaji wa taarifa za tenda husika

Wazabuni wengi wamelalamika kuhusu kupokea majibu mabaya wanapokuwa katika ofisi za waliotangaza tenda kutafuta taarifa za tenda husika, haswa kutoka kwa walinzi wa ofisi hizo. Yawezekana sababu ni kwamba walinzi wamekuwaa wanapewa maelekezo ya kutomruhusu mtu yeyote asiye na shughuli maalumu kuingia ofisini kirahisi ili kuepusha usumbufu, na mara nyingi mzabuni (au mtafuta tenda) anaonekana kama mtu anaetafuta kazi hivyo huzuiwa kuongea na wahusika.

Lakini pia pia idara husika ya manunuzi (procurement department) imekua haiweki mawasiliano yao wazi kwa ajili ya kuulizwa maswali zaidi au kutoa uelewa na tena wakipigiwa mara kwa mara na watu tofauti kuulizwa swali lile lile hawapokei simu au kutoa ushirikiano unaoeleweka.

Na hii ni moja kati ya vitu ambavyo vimekuwa vikiwakatisha tamaa wazabuni wengi sana. Je, ufanyaje unapokutana na changamoto kama hiyo;

Usikubali kupokea majibu mepesi kwa mambo mazito yanayohitaji umakini kutoka kwa mtu ambaye unadhani haelewi kile kitu unachokitaka. Unapofika katika ofisi husika kuomba taarifa Zaidi, sisitiza kukutana moja kwa moja na watu wa manunuzi kwa kuwa wao ndo wanaweza kuyajibu maswali yako vizuri zaidi.

Unaweza kubadili mfumo wako wa utafutaji tenda, jaribu njia mbali mbali za mtandaoni kama vile jukwaa la Zabuni app. Huku utapata taarifa nzuri zaidi, kwa urahisi na haraka iwezekanavyo kuhusu tenda iliyotangazwa kwa kupakua tu hati ya tenda husika. Lakini pia unaweza kuwasiliani nasi pale unapokwama tuone namna gani nzuri ya kuwafikia waliotangaza tenda ili waweze kukusaidia.

HITIMISHO

Changamoto ni sehemu ya Maisha na usikubali hata siku moja zikufanye ushindwe kutimiza malengo yako. Unaweza kutembelea Zabuni app au https://zabuni.co.tz ili uone ni jinsi gani jukwaa hili linaweza kukurahisishia jitihada zako za utafutaji tenda hapa nchini Tanzania.