Spread the love

ukiwa kama mwanzilishi wa kampuni changa yawezekana hauna uzoefu mkubwa katika suala zima la kuomba zabuni, hivyo kuna vitu yawezekana unavikosa au huvijumuishi kaztika zoezi zima la uombaji tenda. Makala hii inalenga kukujulisha mambo makuu na muhimu kabisa ambayo hutakiwi kuyaacha kila uombapo zabuni katika taasisi mbalimbali:

 

Mosi; mtangaza Zabuni tayari ana budget ya kile unachotaka kuomba kukifanya kama ni kutoa huduma ama bidhaa. Hivyo unaweza ukafanya uchunguzi wa vile vitu unataka kuvifanya vitagharimu kiasi gani ukiwa umeweka na bei ya usafirishaji, bei ya ongezeko la thamani ‘VAT’, faida ya kampuni yako kadhalika.

Sasa hapa wengi ndio hutaka wapate faida mara dufu kwenye kazi moja, anaweka bei ambayo ni ngumu kwake kupita kwenye mchujo wa awali. Sasa jitahidi kujaza bei ambayo ni realistic, ili wakiiona uwe miongoni mwa wanaofikiriwa kupewa kazi. Ukizingatia wanaangalia thamani ya pesa (BEST VALUE FOR MONEY ‘BVM’), muda unaoweza kutumia kutoa huduma ile au bidhaa, uwezo wako, uzoefu kadhalika, ila kikubwa ni thamani ya pesa.

 

Pili; Zabuni nyingi zenye pesa nzuri hasa hasa zinazotsngazwa na taasisi za umma zinakuwa na ushindani wa hali ya juu. Kiasi kwamba kwa kampuni changa zinazoanza inakuwa ni nadra sana kwao kuweza kupata kazi zile. Kwa sababu ya ukomavu wa kifedha (financial statements), uzoefu katika kufanya kazi ikle au huduma, na mambo kadha wa kadha.

Lakini pia wanasahau kuwa kuanza na kazi ndogo ndogo ( ninamaanisha kazi zenye thaani ya pesa ndogo) ambazo nyingi huwa ni kutoka katika taasisi binafsi, taasisi ziso za kiserikali ( private companies and Non-Govermnatal  Organizations [NGOs]) mara nyingi huwa zinatangaza kazi zenye thamani ya mfano Tsh. 2,000,000 hadi labda Tsh. 10,000,000/=

Sasa kampuni nyingi changa hazitilii maanani kazi za namna hii wanakimbizana na zile zenye thamani kubwa ya pesa ambapo ushindani wake pia ni mkubwa.

 

Miongoni mwa mambo mawili na makubwa na ya muhimu ya kuzingatia kwa kampuni changa zinapokuwa zinaomba Zabuni katika taasisi mbalimbali ni kuwa kampuni hizi sasa zinaweza kuangalia upande mwingine wa sekta binafsi na NGOs ili kuanza kujenga jina kwa kufanya kazi za namna hjii ambazo ukitafuta kazi kwa bidii unaweza kupata hadi kazi 4-5 kwa mwaka ambazo zikakuweka katika hali nzuri ya kuishindani lakini pia profile ya kampuni inaanza kuwa ya kueleweka.

HITIMISHO

Kama muasisi wa kampuni changa, unaweza kukutana na vikwazo vingi sana wakati wa kusaka tenda mbalimbali na vingi vikitokana na kukosa kwako uzoefu mkubwa sokoni. Hili lisikutie wasiwasi, kuna mambo mengi unaweza kuyafanya ili kujiweka katika nafasi ya kuzifanya huduma zako zionekane bora Zaidi kwa ajili ya mteja wako.pia jaribu njia mbalimbali za kutafuta tenda kama vile tovuti za mtandaoni na kadhalika ili kurahisisha mchakato wako. Unaweza tembelea tovuti kama zabuni app ambayo inaorodhesha tenda zote Tanzania kutoka serikalini na mashirika binafsi hapa.