Spread the love

 Kwa kampuni zinazoanza au ambazo zipo muda mrefu lakini uwezekano wa kupata kazi zinazotangazwa na taasisi binafsi na NGOs tutakubaliana kuwa vyanzo vyake vya kifedha havijakaa vizuri, kwa maana wanatumia tu pesa kuomba kazi zile, ufuatiliaji, kutunza kampuni lakini wanachokiingiza kwa muda huo huwa ni kidogo sana au hakuna kabisa.

Lakini pia kampuni nyingi za namna hii utazitukuta maeneo ya nje na miji mikumbwa ambapo wakati mwingine kupata taarifa za Zabuni mpya kutoka taasisi binafsi huwa zinapata zinapatikana kwa kuchelewa kutokana na umbali, kutokuwa karibu na vyanzo haswa, au kuona taarifa zile wakiwa wamechelewa kutokana na mawasiliano kuwa shida wakati mwingine au huduma ya internet kuwa duni na gharama kuwa kubwa za uendeshaji.

Sasa basi, yapo maeneo ambapo kampuni changa zinaweza kuwekeza nguvu zaidi ili kuweza kuona fursa mbalimbali zitangazwazo na taasisi binafsi pamoja na NGOs mbalimbali nchini Tanzania.

 

MAGAZETI

Hii ni mojawapo ya njia ya kupashana habari mbalimbali zikiwemo za Zabuni mbalimbali. Kwa taarifa zilizopo; Tanzania magazeti makubwa 33 na meingine zaidi ya 116 yakiwemo ya dini na taasisi mbalimbali binafsi na za umma.

Changamoto ni kuwa itakuwa gharama sana kununua magazeti kila siku ukiangalia nani katangaza Zabuni leo. Na hata kwa maeneo mengine huduma ya magazeti inakuwa haifiki kwa uhakika.

 

MAJUKWAA YA MTANDAONI

Haya ni majukwaa mbalimbali ambayo hutoa taarifa za kuwepo kwa Zabuni mbalimbali, wengi hutegemea kutoa kwenye magazeti, wngine hutoa sio tu kila mara bali mara chache chache kulingana na namna yao ya upataji hizo taarifa. Mengine huwa ya kulipia, mengine huwa ni bure. Lakini pia suala la internet na gharama zake kwa baadhi ya kampuni changa huwa ni changamoto kidogo kuingia kwenye tovuti kuangalia nani katangaza nini leo.

 

ZABUNI APP & ZABUNI TOVUTI.

Huu ni mtandao ambao ulianzishwa mwaka 2019 nchini Tanzania ukiwa na makazi yake Jijini Dr es Salaam katika ofisi za Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Commission for Science and Technology- COSTECH).

Ni mfumo ambao unakusanya Zabuni kadha wa kadha kutoka taasisi za umma, TAASISI BINAFSI, NGOs, mashirika ya kimataifa yenye ofisi ndogo nchini Tanzania. Ni mfumo ambao ukiwa na simu ya smartphone ya Android waweza kupakua app ya Zabuni kutoka katika Google Play Store kwa jina la ZABUNI. Alafu kujisajili ni rahisi na matumizi yake ni rahisi pia ambapo mtumiaji anapata pia tender document ikiwa imeambatanishwa pale, ikiwa na maelezo ya awali ya Zabuni ile, mawasiliano ya mtangaza Zabuni ile na mambo wa kadha.

Lakni pia ZABUNI TOVUTI ( https://zabuni.co.tz )ni mtandao ambapo kwa kutumia laptop au desktop ni rahisi kuingi kwenye mfumo ule na kuweza kujisajili na kutumia. Unatoa huduma kama ambavyo Zabuni App inatoa ikiwemo Zabuni kutoka taasisi za umma, binafsi, NGOs na kadhalika.

Ni mfumo rahisi na rafiki kuutumia ambao kuanzia 2019 mwishoni hadi Januari 2022 umeweza kutangaza jumla ya Zabuni 10650 na watumiaji zaidi ya 4,000 ndani na nje ya nchi. Na ni mtandao ambao watu wametoa shuhuda kadhaa za kuweza kunufaika nao na kupata Zabuni wengi wakithibitisha wamepata kutyoka kwenye taasisi binafsi na NGOs. Ni mtandao wa kuaminika unaotangaza Zabuni kila siku ya Jumatatu hado Jumamosi isipokuwa siku za sikukuu.

Kwa kuhitimisha, kama kichwa cha habari kinavyoeleza, kampuni nyingi changa na ambazo zimenaza muda mrefu ila zinadorora; zinaweza kutazama upande wa Zabuni zinazotangazwa na taasisi binafsi na NGOs kwani ushindani wake sio mkubwa sana, nyingi ni za bei isiyo kubwa sana, lakini pia wanapotangaza zabuni wana uhakika wa kulipa kwa wakati pindi unataka kutoa huduma na unapomaliza kuliko kusubirishiwa malipo yako kwa muda wa miezi zaidi ya mitatu kama baadhi ya  taasisi za umma.

Lakini pia mazingira ya rushwa ni adimu kwani wataangalia kile umekiandika kama kinakidhi vigezo upo kwenye nafasi nzuri ya kushinda Zabuni ile. Lakini pia haina mazingira makubwa ya unamjua nani pale, ukiweza kuandika andiko lako vizuri na kitaalamu kupata Zabuni ni kazi nyepesi sana.

Mwisho kabisa  kupata taarifa au kuomba Zabuni nyingi za taasisi za binafsi na NGOs na mashirika ya kimataifa yenye makazi nchini Tanzania huwa hazilipiwi, kwa maana nyingi ya Zabuni zile huwa ni bure kabisa kuomba au kama kuna ada ya kulipia huwa  ni ndogo sana na himilivu.

Mfumo wa Zabuni unaweka taarifa mbalimbali za Zabuni mbalimbali zinazokuwa zinatangazwa na taasisi  binafsi, NGOs na zile za nje zenye makazi hapa nchini katika vipengele kama vile;

– Civil & building works

– Hotel goods & services supplies

– Medical Equipment supplies

– Catering services

– Construction materials supplies

– Electrical materials supplies

– Spare parts supplies

– Cleaning services

– Consultancy works

– Vehicle & Machinery supplies

– Utility works

– TANESCO supply equipment

– Fumigation works

– Non-consultancy works

– Printing & Stationery supplies

– Oil, fuel & lubricants supplies

– Debt & Auctioning works

– Repairs & maintenance

– ICT equipment supplies

– Safety & security supplies

– Mining Tenders

– Food & agricultural supplies

– Office equipment supplies

– ICT services provision

– SPECIAL GROUPS Tenders

– Insurance services

– Freight, Clearing & Forwarding Works

Bila shaka andiko hili limekupa mwanga wa namna bora KAMPUNI CHANGA kama ya kwako zinazoanza zinavyoweza zinavyoweza kunufaika kwa KUTOA HUDUMA AU BIDHAA kwenye taasisi zingine binafsi na NGOs nchini Tanzania.